
Historia Fupi Kuhusu Amani Kwaya
Amani Kwaya ni huduma ya uimbaji wa nyimbo za Injili iliyoanzishwa tarehe 20/12/2002 ikiwa na idadi ya watu sita(06) chini ya mwalimu wa kwaya Catheline Kishai na kwaasa wamekuwa na idadi ya watu(25) huku ikiwa na mwalimu Dickson Stevene na viongozi wafuatao mwenyekiti Julius Zima,mwenyekiti msaidizi Rose Ngonyani,katibu Caroline Jeremiah,na muweka hazina Reticia Mushi na huku ikilenga kugusa mioyo ya watu na kueneza neno la Mungu kupitia njia ya uimbaji kote duniani.
Huku tukiongozwa na kaulimbiu yetu : Mwanzo 26:22 REHOBOTHI (kwa kuwa BWANA ametufanyia nafasi).
Maono Yetu (Vision)
Kuwa chombo kikuu cha injili kupitia uimbaji, kikigusa na kubadilisha maisha ya watu kiroho na kimwili ulimwenguni kote.
Malengo Yetu
- Kuhubiri Injili ya Yesu Kristo kupitia nyimbo zenye ubora na ujumbe wa uzima.
- Kuinua na kukuza vipaji vya uimbaji na kuwasaidia au kuwafikia wahitaji.
- Kushirikiana na makanisa pamoja na huduma mbalimbali katika matamasha na mikutano ya injili.